Thursday, November 24, 2011

MWANAMME ALIYEJIGEUZA DEMU AZUA HOFU DUNIANI


ONEAL Morris, dume  aliyebadili jinsi yake amezua hofu duniani kufuatia picha zake za kwenye mtandao zikimwonesha ni mwanamke, ‘pyua’.
Baadhi ya watu waliotoa maoni kwenye mtandao ulioanika picha za Oneal wamesema wanaamini dunia imefika ukingoni na sasa ni wakati wa bindamu kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

WANAFUNZI WAKODI MABASI KWENDA SHOO YA SUGU.....

SHOO ya uzinduzi wa mix-tape ya Anti Virus inazidi kubamba, upo uwezekano ikajaza nyomi ambalo halijawahi kutokea kutokana na ahadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kwamba watakodi mabasi kwenda kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar.

Anti Virus itasababishwa na Vinega Novemba 26, 2011, kuanzia saa 12 jioni mpaka 6:00 usiku na katika kuhakikisha wanashuhudia makamuzi ya maana, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, wameahidi kukodi m
abasi matatu ya kuwasafirisha kwenda kwenye shoo hiyo.


INABIDI TUKIMBIE WAKATI WENGINE WAKITEMBEA....

Lakini pia ni lazima tukumbuke kwamba wakimbiao huchoka mapema kuliko watembeao, na kama ni mbio za masafa marefu na wakimbiaji hawa wakawa hawajajiandaa na kuchunguzwa afya zao vizuri ipo hatari ya kupata mshtuko wa moyo na kufikwa na umauti wa ghafla. Ati kama ni lazima tupige mbio, sisi tumejiandaaje? Tunajua tuendako? Basi tusije tukakurupuka na kuanza kupiga mbio kama wendawazimu!