Thursday, November 24, 2011

MWANAMME ALIYEJIGEUZA DEMU AZUA HOFU DUNIANI


ONEAL Morris, dume  aliyebadili jinsi yake amezua hofu duniani kufuatia picha zake za kwenye mtandao zikimwonesha ni mwanamke, ‘pyua’.
Baadhi ya watu waliotoa maoni kwenye mtandao ulioanika picha za Oneal wamesema wanaamini dunia imefika ukingoni na sasa ni wakati wa bindamu kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.


Aidha, baadhi ya watoa maoni hao waliwaonya wanaume ambao hawajaoa kuwa makini kwani kuna uwezekano wa kumchumbia mwanaume aliyebadili jinsi yake.
“Unajua tabia ya kukutana na mwanamke ukamuingiza ndani bila ya kumchunguza tutakuja kuoa madume jamani! Si mmemuona huyu, ana tofauti gani na mademu wengine? Amejaliwa kila idara,” alisema msomaji mmoja wa mtandao huo.

Mbali ya kujibadili jinsi, hivi karibuni Oneal  alitiwa mbaroni na polisi wa Florida nchini Marekani kwa kosa la kuwabandika wanawake makalio ya bandia akitumia simenti, gundi (super-glue) na mafuta ya petrol.
Aidha, ‘demu’ huyo anashitakiwa kwa kumsababishia  matatizo mwanamke mmoja aliyemchoma sindano ya kuongeza makalio ambaye kwa sasa yuko chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kufuatia mabadiliko hayo.  

No comments:

Post a Comment