Monday, May 28, 2012

SAVING UNDERGROUND ARTIST S.U.A


Freestyle Battle ikachukua nafasi pande za Kijenge, Arusha Tanzania.
Mwanzilishi wa S.U.A Daz Nalegde ambaye pia ni producer wa Watengwa alizindua Shoo.
Ma mc's walikuwa wa kutosha kina Jaco b, Ghosti b, Donnii, Sight Mo na wengine kibao......!

MACHAFUKO ZANZIBAR

Kiongozi wa Jumuiya ya kikundi cha uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed

 


MAKANISA YACHOMWA, WABARA WATAKIWA KUONDOKA
ZANZIBAR imechafuka. Baada ya kuwapo kwa amani kwa takribani mwaka mmoja tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, vurugu na hali ya wasiwasi zimeibuka tena baada ya wanaharakati wa Kiislam kufanya maandamano kutaka uhuru wa visiwa hivyo. Zanzibar ilijikuta katika hali tete kiusalama tangu mwaka 1995 baadaya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) kiilibuka kidedea na Chama cha Wananchi (CUF) kupinga, lakini uhasama huo ulizikwa Julai 31 mwaka 2010, baada ya kura ya maoni ya kuunda Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa. Lakini kuanzia juzi usiku hadi jana jioni mji wa Unguja na viunga vyake ulitikiswa na mabomu ya kutoa machozi ambayo polisi waliyatumia kutawanya mamia ya wanaharakati hao wa Kiislam wakiongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Mabomu ya machozi yalipigwa mfululizo juzi usiku na kuendelea kutwa nzima jana, hivyo kuathiri shughuli za biashara, ibada katika makanisa mbalimbali na kusababisha hofu kwa wananchi. Kwa muda wa saa takriban mbili hivi kati ya saa 3:00 na saa 5:00 asubuhi, helkopta ya polisi ilikuwa ikipasua anga la Zanzibar ambalo lilikuwa limetandwa na moshi uliotokana na mabomu ya machozi pia uchomaji wa matairi ya magari. 
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba, watu saba akiwamo Imamu wa Msikiti wa Bizeredi, Maalim Mussa Juma wanaotuhumiwa na matukio hayo wamekamatwa na jeshi hilo.
 

Thursday, May 24, 2012

JOHN MNYIKA ASHINDA KESI YA UCHAGUZI JIMBO LA UBUNGO

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili ya uchaguzi wa jimbo hilo wa mwaka 2010, baada ya Mahakama kutupilia mbali mashitaka yote matano yaliyokuwa yakimkabili ambayo ni :
1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)
Mlalamikaji Hawa Nghumbi (CCM) anatakiwa kulipa gharama zote za kesi hiyo kama ilivyoamriwa na Mahakama.

Wednesday, May 23, 2012

WABUNGE WATARAJIA KUTOA NYIMBO


Zitto Kabwe

 Vicky Kamata


 January Makamba


Halima Mdee

Zitto Kabwe, Halima Mdee, January Makamba, Vicky Kamata na Esther Buraya wanatarajia kutoa nyimbo.
Wabunge hao ndio vijana wanaotutetea kama walivyotajwa hapo juu wako studio tayari kwa kuachia ngoma ambayo nahisi itakuja kubamba vilivyo. Ndani ya ngoma hiyo ambayo zitasikika sauti za wabunge hao tu kutakuwa na ujumbe wa kuhamasisha vijana na maisha ya sasa na pia kuwapa changamoto ambazo zitaweza kuwasaidia kupambana na maisha yanayoendelea duniani.

Monday, May 21, 2012

WATENGWA AT FRANCE REPRESENT HIP HOP



Watengwa 2 France is a cultural exchange program between Tanzania and France part of East Africa Rise Up (EARU) Project.
EARU project was started in 2006 in partnership with a french organization calledUUKSA. Since 2010, UUKSA organizes a music festival called Festiv'Al Arrach near Paris in France in order to support EARU project.
EARU project was started in 2006 in partnership with a french organization calledUUKSA. Since 2010, UUKSA organizes a music festival called Festiv'Al Arrach near Paris in France in order to support EARU project.
Keep it real WATENGWA the hardcore unit represent real Hip Hop from Tanzania Arusha Kijenge Juu .........!
FULL ILE LAANA VOL II

Sunday, May 20, 2012

CHELSEA WACHUKUA KOMBE LA UEFA

Chelsea imetwaa ubingwa Ulaya baada ya kuifunga Bayern Munich mikwaju ya penalti 4-3 mchezo wa fainali uliopigwa Allianz Arena. Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za kawaida, Drogba ambaye yuko njiani kutemwa na klabu hiyo kwa kuwa ni 'mzee' alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 83 na kufunga penalti ya mwisho iliyoamua bingwa.
Drogba ni kama nyota wa mchezo ambaye anasema: "Ni jitihada zetu, tulijipanga muda mrefu na sasa matokeo yake yameonekana. Tumecheza kwa tahadhari lakini kwa kujiamini, tuliondoa hofu ya mchezo na tulipambana hadi mwisho.

Ubingwa wa Chelsea ambao ni wa kwanza katika historia ya kombe hilo na klabu, umemaliza hasira za timu hiyo kushindwa katika fainali ya 2008 walipopoteza mechi kwa Manchester United kwa mikwaju ya penalti 6-5 mjini, Moscow Russia.Chelsea iliyokuwa bila nahodha wake, John Terry, anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyozawadiwa kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Barcelona ilikuwa makini katika mchezo huo licha ya kutangulia kufungwa.

Mpachika mabao mahiri, Thomas Mueller aliifungia Bayern Munich bao la kuongoza katika dakika ya 83. Toni Kroos alipiga mpira kutoka wingi ya kulia na kumchanganya Mario Gomez na Ashley Cole na mpira kumkuta Thomas Mueller aliyeutupia ndani ya kimia. Dakika ya 88, Didier Drogba ambaye anakwenda China kucheza soka ya kulipwa na Nicolas Anelka katika klabu ya Shanghai Shenhua, alifunga kwa kichwa katika dakika ya 88.

Baada ya hapo, zilifuata dakika 120, na waliokuwa wamalize mchezo mapema ni Bayern Munich lakini Arjen Roben alikosa penalti iliyodakwa na kipa Petr Czech. Ilipowadia wakati wa mikwaju ya penalti, Bayern Minich waliotwaa kombe hilo mara nne 1974-76 na 2001, walifunga tatu za kwanza kupitia kwa Philipp Lahm, Mario Gomez na  Manuel Neuer wakati Juan Mata na Bastian Schweinsteiger walikosa.
Walioifungia Chelsea ni David Luiz, Frank Lampard, Ashley Cole na Didier Drogba wakati Ivica Olic alikosa penalti yake. Drogba ndiye aliyesawazisha na kisha kufunga penalti iliyoipa ubingwa timu hiyo.
TIMU ZA ENGLAND ZILIZOWAHI KUWA BINGWA WA ULAYA:
Liverpool (Mara 5)
Manchester United (3)
Nottingham Forest (2)
Aston Villa (1)
Chelsea (1)

Monday, May 14, 2012

MANCHESTER CITY BINGWA EPL


Baada ya miaka 44 hatimaye Man City wamechukua ubingwa wa England 2012 maarufu kama English Premier League, baada ya kuifunga Queens Park Rangers magoli 3-2. Mshambuliaji Sergio Aguero alifunga bao la tatu na ushindi katika dakika za majeruhi na kurudisha shangwe za mashabiki wa City uwanjani hapo.
Zabaleta alifunga bao la kwanza kabla ya Edin Dzeko na Aguero waliokuwa mashujaa wa City kwenye uwanja wake wa Etihad kufunga mabao. "Kushinda kwa aina hii ni kitu kizuri. Sijawahi kuona mechi ya mwisho ngumu kama hii. Baada ya miaka 44 tumefanikiwa kutoa zawadi kwa mashabiki wetu wote," alisema kocha wa City, Roberto Mancini.

Sunday, May 6, 2012

FLOYD MAYWEATHER AMPIGA MIGUEL COTTO


FLOYD 'MONEY' MAYWEATHER ampiga MIGUEL COTTO kwa points..also takes Cotto's WBA Super Welterweight title, and remains undefeated at 43-0-0 record.

SIMBA SC YACHUKUA UBINGWA KWA KISHINDO' YAMPIGA YANGA 5-0

Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma Kaseja Juma kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa  kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii  kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo.
Kikosi cha Simba Football Club

Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza.nGoli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga  goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari. 

CHELSEA YATWAA KOMBE LA FA

Saturday, May 5, 2012

RAIS KIKWETE ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI



Rais Jakaya Kikwete hivi punde ametangaza Baraza jipya la Mawaziri likiwa na sura mpya wakati baadhi ya Mawaziri wakibaki katika nafasi zao. Ifuatayo ni orodha ya Mawaziri hao walioteuliwa pamoja na Manaibu Waziri.
 Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo Aprili 4, 2012.Rais Jakaya Kikwete hivi punde ametangaza Baraza jipya la Mawaziri likiwa na sura mpya wakati baadhi ya Mawaziri wakibaki katika nafasi zao. Ifuatayo ni orodha ya Mawaziri hao walioteuliwa pamoja na Manaibu Waziri.

Tuesday, May 1, 2012

MATOKEO KIDATO CHA SITA NJE NJE

Matokeo ya kidato cha sita 2012 yametoka wapendwa.

Click  kwenye link hapa chini;
http://utawala.udsm.ac.tz/form62012/Alevel.htm


BARAZA la Mtihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita iliyofanyika Februari mwaka huu yakionyesha kuongezeka kidogo kwa kiwango cha ufaulu kwa ujumla huku wavulana waliofaulu wakiwaacha