Friday, May 3, 2013

MATOKEO YA FORM IV 2012 KURUDIWA KUPANGWA UPYA

Hatimaye Serikali imefuta matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2012 kufuatia asilimia 65.5 ya Wanafunzi wote waliofanya mtihani huo kupata daraja sifuri na kupelekea kuundwa kwa Tume ya Taifa ya kuchunguza suala hilo.
Akitoa kauli ya Serikali Bungeni kuhusu taarifa ya awali ya tume hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI amesema, kiwango cha ufaulu kimeanza kushuka mwaka 2008 kuliko miaka iliyotangulia.
Kufuatia mapendekezo ya Tume ya Taifa ya kuchunguza matokeo hayo, tayari Baraza la Mawaziri limeridhia uamuzi huo na kutaka mapendekezo yote ya tume hiyo yaanze kutekelezwa mara moja.Katika kuweka kumbukumbu za matokeo ya mtihani huo sawa LUKUVI anataja changamoto ambazo zimechangia idadi kubwa ya Wanafunzi kupata daraja sifuri.
Kati ya wanafunzi 367,756 waliofanya Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2012 watahiniwa 126,847 walifaulu ambapo 23, 520 pekee ndio waliopata daraja la kwanza hadi la tatu.
Taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne imesomwa bungeni leo na Mh Lukuvi, amesema sababu zilizosababisha wanafunzi wafeli ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu ya kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na utaratibu mmbovu wa baraza la mitihani uliotumika bila kuwashirikisha wadau wa elimu. Mh Lukuvi amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATION AND CONTINUOUS ASSESSMENTS.
Hivyo basi, matokeo hayo yamefutwa na yatapangwa upyaaa.
Hii imekua habari njema na nzuri kwa wale wanafunzi walio wengi na waliofeli mitihani hiyo ya form iv mwaka jana 2012.

link 2, moja ya website yao ya Necta, na link ya pili ni page yao katika mtandao wa kijamii wa facebook; 

AY FT FID Q - JIPE RAHA