Tuesday, October 25, 2011

WATU 14 WAJERUHIWA KATIKA SHAMBULIO NAIROBI

Watu wa Usalama wakikagua ndani ya klabu hiyo.


Damu ikiwa imetapakaa katika klabu hiyo

WATU wapatao 14 wamejeruhiwa katika shambulio la guruneti  lililotokea jana majira ya saa 7 usiku katika klabu ya Mwaura iliyopo mjini Nairobi, nchini Kenya.  Imeripotiwa kuwa guruneti hilo lilirushwa na mtu asiyejulikana. Mtu huyo alifika kwenye eneo hilo la burudani na mlango ulipofunguliwa alirusha guruneti na kutokomea. "Jamaa mmoja aligonga mlango akijifanya kama mteja na aliporuhusiwa kuingia ndani, akarusha guruneti"  alisema mkuu wa polisi mjini Nairobi, Bw. Anthony Kibuchi. Wengi wa majeruhi wa tukio hilo walikuwa na majeraha katika sehemu za mikono na miguu na walikimbizwa katika hospitali kuu ya taifa ya Kenyatta. Shambulio hili linatokea wiki moja baada ya vikosi vya Kenya kuingia nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa al-Shabaab, ambao Kenya inawashutumu kwa mashambulio na utekaji nyara wa watalii. Al-Shabaab walitishia kufanya mashambulio kutokana na hatua hiyo ya Kenya.

AMAZING FACTS ABOUT GADDAFI


Muammar Abu Minyar al-Gaddafi.

1. There is *no electricity bill* in Libya; electricity is free for all its citizens.
2. There is *no interest on loans*, banks in Libya are state-owned and loans given to all its citizens at 0% interest by law.
3. *Home* considered a human right in Libya – Gaddafi vowed that his parents would not get a house until everyone in Libya had a home. Gaddafi’s father has died while him, his wife and his mother are still living in a tent.
4. All newlyweds in Libya receive *$60,000 Dinar* (US$50,000) by the government to buy their first apartment so to help start up the family.
5. Education and medical treatments are free in Libya. Before Gaddafi only 25% of Libyans are literate. Today the figure is 83%.
6. Should Libyans want to take up *farming* career, they would receive farming land, a farming house, equipments, seeds and livestock to kick-start their farms – all for free.
7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need in Libya, the government funds them to *go abroad* for it – not only free but they get US$2,300/mth accommodation and car allowance.
8. In Libyan, if a Libyan buys a *car*, the government subsidized 50% of the price.
9. The price of *petrol* in Libya is $0.14 per liter.
10. Libya has *no external debt* and its reserves amount to $150 billion – now frozen globally.
11. If a Libyan is unable to get *employment* after graduation the state would pay the average salary of the profession as if he or she is employed until employment is found.
12. A portion of Libyan *oil sale* is, credited directly to the bank accounts of all Libyan citizens.
13. A mother who *gave birth* to a child receive US$5,000
14. 40 loaves of *bread* in Libya costs $ 0.15
15. 25% of Libyans have a *university degree*
16. Gaddafi carried out the world’s largest *irrigation* project, known as the Great Man-Made River project, to make water readily available throughout the desert country.
Which other dictator has done much good to his people besides.
*P.S.  If this is the dictator Gaddafi is, then give us one like him here in Bolehland.

Monday, October 24, 2011

MAN U YAPATA KIPIGO 6-1 DHIDI YA MAN CITY

MANCHESTER UNITED JUMAMOSI ILIGEUKA NA KUWA MANSITA
Baada ya kupokea kichapo toka kwa mahasimu wao Manchester city, kwenye uwanja wao wa nyumbani Old Trafford  OT.

Mchezo wa Manchester United umeacha majonzi makubwa si tu katika jiji la Manchester bali ni kwa wapenzi wa timu hiyo walioko dunia nzima waliposhuhudia bila kuamini timu yao ikichapwa mabao 6-1 huku Mario Balotelli akipachika magoli mawili.
Sergiao aliongeza bao la tatu kwa Man City na kuimarisha ushindi wao wa kishindo kwenye uwanja huo tangu waliposhinda 6 -1 January 1926.
David Silva alifunga la nne huku mawili ya mwisho yakipachikwa na Edin Dzeko, na Man U walipata la kufutia machozi lililowekwa kambani na Fletcher. Hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa Jonny Evans wa United kupewa kadi nyekundu.

Saturday, October 22, 2011

MZOZO JUU YA MAZISHI YA GADDAFI.

Mazishi ya Kanali Muammar Gaddafi yamesitishwa kutokana na tofauti zilizozuka baina ya maafisa wa Libya kuhusu jinsi ya kufanya maziko hayo. Chini ya utamaduni wa Kiislam, maziko hutakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo. Lakini waziri wa mafuta wa Libya amesema mwili wa Gaddafi huenda ukahifadhiwa "kwa siku kadhaa".Haifahamiki kama kiongozi huyo wa zamani atazikwa Sirte, mji aliouawa siku ya Alhamis, au Misrata, mji aliopelekwa baada ya kufa, au mahala pengine.Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kifo cha Muammar Gaddafi kinamaanisha shughuli za Nato nchini Libya zimefikia kikomo.Awali kulikuwa na taarifa kuwa mamlaka nchini Libya zinafanya mipango ya kufanya mazishi ya siri kwa kiongozi huyo. Hata hivyo, inaonekana huenda kukawa na kuchelewa kufanyika kwa mazishi hayo, ambayo chini ya utamaduni wa Kiislam mazishi hufanyika haraka iwezekanavyo.Waziri wa mafuta Ali Tarhouni aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mwili wa Kanali Gaddafi huenda ukahifhadhiwa "kwa siku kadhaa".

JAMAA ANA WAKE 39, WATOTO 94 NA NYUMBA YENYE VYUMBA 100

Familia yake inaendeshwa kwa utawala unaofanana na kijeshi huku mke mkubwa mwenye umri wa miaka 69 akiwa mpangaji mkuu wa majukumu ya uendeshaji nyumba kwa wenzake , mlo wa siku ni karibu gunia zima la mchele na kuku wapatao 30.
Nyumba ia Ziona ina uwanja wa kuchezea watoto,mabanda ya kufugia wanyama ,shule yake yenyewe na sehemu ya uhunzi. Kuna wakati alioa wake kumi katika mwaka mmoja na chumbani kwake ana sita kwa sita la kufa mtu na kila usiku mke mmoja huwa naye ,hivyo huwachukua kila mtu zaidi ya miezi miwili kwa wake zake kuwa naye faragha ya usiku. vyumba vya wake zake wadogo viko karibu na chumba chambe na walio wazee viko mbali naye.
Ziona na Wake zake
Jumba la ZIONA


Friday, October 21, 2011

MWISHO WA GADDAFI


ALIYEKUWA kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi ameripotiwa kuuawa na wapiganaji wanaoongozwa na Baraza la Mpito nchini humo (NTC), baada ya mji wa nyumbani kwake, Sirte kunyakuliwa na vikosi hivyo jana.Kifo cha Kanali Gaddafi (69) kilitangazwa rasmi na Waziri Mkuu wa Serikali ya mpito nchini humo, Mahmoud Jibril, muda mfupi baada kiongozi huyo aliyeitawala Libya kwa miaka 42 kuuawa. Awali, msemaji wa NTC nchini Libya, Kanali Ahmed Bani alisema Kanali Gaddafi aliuawa na mwili wake ulipelekwa katika mji wa Misratah, bila kutoa ufafanuzi kamili kuhusu mazingira ya kifo hicho.Taarifa za kuuawa kwake zilitolewa huku zikiambatanishwa na picha zinazoonyesha sura inayoonekana kuwa ni ya kiongozi huyo, katika muonekano wa nywele zake laini na ndefu wastani na uso uliotapakaa damu na majeraha.Kanali Gaddafi anakuwa kiongozi wa kwanza kuuawa tangu kuanza vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya kiarabu mwanzoni mwa mwaka huu, yaliyowaondoa madarakani Rais Ben Ali wa Tunisia na Hosni Mubarak wa Misri.Kifo hicho kimetangazwa ikiwa ni miezi tisa tangu kuanza kwa upinzani mkali dhidi ya Serikali yake Februari mwaka huu, ambapo aliapa kwamba asingeondoka nchini Libya na kwamba yeye na wafuasi wake wangepambana hadi tone la mwisho la damu.Kanali Gaddafi ambaye wakati wa utawala wake aliwahi kujipa wadhifa wa “mfalme wa wafalme wa Afrika” alikuwa akisifika kwa ukali wa sauti yake na maneno makali ya kuhamasisha na kueleza misimamo yake katika hotuba zake. Mapambano hayo yameishia katika mji wa nyumbani kwake, Sirte ambao umekuwa na upinzani mkali kwa vikosi vya wapiganaji wa NTC ambavyo vililazimika kupambana kwa miezi kadhaa hadi waasi walipofanikiwa kuuteka jana. Kanali Bani alisema mtoto wa Kanali Gaddafi, Mutassim ambaye walikuwa pamoja katika mji wa Sirte aliuawa na wapiganaji hao wa NTC. Msemaji huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa kiongozi huyo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya katika miguu yake yote na kichwani. “Aliuawa katika mapambano na wapiganaji wetu. Kuna picha zinazoonyesha hayo,”alisema.Alijificha kwenye karavatiKwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, Kanali Gaddafi alidhibitiwa baada ya kukutwa  amejificha katika karavati la barabarani, yeye pamoja na baadhi ya walinzi wake.Kwa upande wake, kamanda wa wapiganaji wa baraza hilo, Abdul Hakim Belhaj pia alithibitisha kuwa Kanali Gaddafi alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kukamatwa.Makamu Mwenyekiti wa NTC, Abdul Hafiz Ghoga alithibitisha mbele ya waandishi wa habari kuwa Gaddafi aliuawa katika mji wa Sirte.“Tunatangaza kwa dunia kuwa Muammar Gaddafi aliuawa katika mikono ya wanamapinduzi,” alisema Ghoga.Katika mtiririko wa matukio yaliyokuwa yakirushwa katika vituo mbalimbali vya televisheni, kituo cha televisheni cha al-Jazeera kilionyesha picha za mwili wa Kanali Gaddafi ukiburuzwa katika eneo alilouawa.Filamu za video zilizochukuliwa kwa simu za mkono zilionyesha kile kilichoonekana kuwa maiti ya Gaddafi iliyolowa damu. Mwili wake baadaye uliburuzwa na wapiganaji na kupakiwa nyuma ya gari aina ya pick-up. Nato na Marekani zilieleza kuwa haziwezi kuthibitisha taarifa za kuuwawa kwa kiongozi huyo ambaye hajaonekana tangu NTC ilipoikamata Tripoli.Watu washangilia mitaaniWakati huohuo, katika mji wa  Benghazi na miji mingine nchini humo, watu walionekana kukusanyika mitaani na kushangilia taarifa hizo za kuuawa kwa Gaddafi.Viongozi mbalimbali duniani pia wamezungumzia kuhusu taarifa hizo za kuuawa kwa Kanali Gaddafi ambaye amewahi kuwa mpinzani mkubwa wa mataifa ya Ulaya na Marekani kutokana na misimamo yake dhidi ya mataifa hayo.Miongoni mwa viongozi hao ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon ambaye alisema ni siku maalum ya kukumbuka maovu yote yaliyofanywa na Gaddafi.Alisema watu wa Libya wako katika nafasi nzuri ya kujenga nchi imara na yenye demokrasia.“Ninafurahi kazi ambayo Uingereza imesaidia katika kuuondoa utawala wa Gaddafi,”alisema.Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Alain Juppe amepongeza kufikiwa mwisho kwa utawala wa miaka 42 ya Gaddafi.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon pia alisema kwamba kifo cha Kanali Gaddafi kinatoa mwanya wa “historia mpya kwa Libya”.“Watu wanatakiwa watambue kuwa huu ni mwisho wa mwanzo. Sasa ni wakati wa Walibya wote kushikamana na kuwa kitu kimoja. Ni wakati wa kuponya majeraha na kujenga upya taifa. Si wakati wa visasi,” alisema Ki-Moon.Balozi wa Libya nchini Uingereza, Mahmud Nacua alisema kuwa kuawa kwa Gaddafi kunamaanisha Libya inaelekea kwenye mustakhabali bora wa baadaye.Wasifu wa Kanali Muammar Gaddafi. Alikuwa mtoto wa wafugaji wa Kibedui, mwenye maisha ya utata, lakini ambaye alitukuzwa sana, huku mataifa ya Magharibi yakimuona mtu wa hatari wakati wote.Muammar Muhammad Gaddafi aliitawala Libya kwa zaidi ya miaka 40. Hadi mwanzoni mwa Machi 2011, alikuwa akiamini ndani ya moyo wake kwamba watu wake walikuwa wakimpenda na kwamba walikuwa tayari kumlinda hadi kufa kwa ajili yake. Lakini wakati huo, tayari Gaddafi alikuwa ameshatumia njia za kikatili kuyazima maandamano dhidi yake, maandamano ambayo baadaye yaligeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa mujibu wa taarifa, watu zaidi ya 30,000 waliuawa kwenye vita hivyo. Mara nyingi sana, Gaddafi alitoa matamko makali wakati wa vita hivyo, ila linalojuilikana zaidi ni lile la kuwaita wapinzani wake kuwa ni panya. Kwa kila hali, yaliyotokea ni mambo ambayo Gaddafi hakuyatarajia asilani. Mtoto huyu wa wafugaji wa Kibedui aliyezaliwa mwaka 1942, alikuja kuibuka kama mkombozi wa Walibya, alipompindua Mfalme Idriss hapo mwaka 1969. Kuanzia hapo akaanza kujenga kile alichokiona mwenyewe kuwa ni mfumo wa kidemokrasia wa moja kwa moja. Alianzisha kamati za umma zilizoamua juu ya mustakabali wa umma na wa Serikali. Aliuita mfumo wake wa kisiasa na kiuchumi kuwa ni wa kisoshalisti, alioufafanua kwenye kijitabu chake cha Kijani.

Wednesday, October 19, 2011

NAKO 2 NAKO FT FUNDI SAMWELI - SWEETY SIXTEEN



KWELI WACHINA NI NOUMER.....!
Charger ya simu yenye uwezo wa kucharge
simu kumi tofauti tofauti kwa wakati mmoja.

HAJI RAMADHANI NDIYE MSHINDI WA BSS 2011, ANYAKUA MILIONI 40


Mshindi wa shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011, Haji Ramadhani (katikati), akipunga mkono kwa mashabiki zake mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang'anyiro hicho (kushoto), ni Mratibu wa mashindano hayo Rita Paulsen 'Madame Rita' akiwa katika pozi mara baada ya kumtangaza mshindi huyo, kulia ni mwakilishi kutoka Tigo ambao walikuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo.
Majaji wa shindano hilo Master J na Madam Ritha wakifurahi.

CABO SNOOP NDANI YA LEADERS CLUB
Cabo Snoop akiwa na dance wake
Lina naye kama kawaida akiwakilisha
pia raia walikuwepo wa kutosha.

Wednesday, October 5, 2011

Steve Jobs Dies: Apple Chief Created Personal Computer, iPad, iPod, iPhone



Steve Jobs, the mastermind behind Apple's iPhone, iPad, iPod, iMac and iTunes, has died, Apple said. Jobs was 56.
"We are deeply saddened to announce that Steve Jobs passed away today," read a statement by Apple's board of directors. "Steve's brilliance, passion and energy were the source of countless innovations that enrich and improve all of our lives. The world is immeasurably better because of Steve. His greatest love was for his wife, Laurene, and his family. Our hearts go out to them and to all who were touched by his extraordinary gifts."
The homepage of Apple's website this evening switched to a full-page image of Jobs with the text, "Steve Jobs 1955-2011."
HIS SOUL REST  IN  PEACE


TPF ALL STARS CONCERT AT NAIROBI
watu waliohudhuria walikuwa wa kutuosha
SHAGGY
CABO SNOOP AKIFANYA VITU VYAKE
Cabo Snoop akimwonyesha EVE mambo ya Windeck Windeck.....!