Tuesday, June 18, 2013

ARUSHA HALI NI TETE' MABOMU NA RISASI ZARINDIMA DHIDI YA WAFUASI WA CHADEMA

Jeshi la polisi mkoni Arusha linapiga mabomu ya machozi na risasi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA pamoja na viongozi wao waliokuwa wamejikusanya katika viwanja vya soweto kuaga miili ya wenzao waliofariki juzi jumamosi kwenye mlipuko wa bomu. Yaani mjini kati ni milio na moshi wa mabomu na milio ya risasi.
Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Tundu Lisu wamekamatwa na jeshi la polisi na wako chini ya ulinzi.
Inaarifiwa kumetokea uaribifu mkubwa wa toyo na baadhi ya magari. Mji haukaliki baadhi ya barabara zimefungwa na watu wanawasha moto katika ya barabara. Maeneo ya Soweto, Sanawari, Stand ndogo, Mianzini na Sabena kote hapafai.

No comments:

Post a Comment