Chanzo
Shuhuda ameeleza kwamba bomu hilo lilirushwa na kijana mmoja ambaye kimwonekano alikuwa ni kijana wa kati ya miaka 20-25, na kwamba baada ya kijana huyo kurusha bomu alikimbia kutoka eneo hilo.
Kukamatwa kwa muhusika
Kuna kijana ambaye alishirikiana na wananchi wengine kumkimbiza mtuhumiwa kutoka Olasiti mlipuko ulipotokea hadi katika kijiji kiitwacho Ndorobo.
Kijana huyo alisimulia kuwa mtuhumiwa alikimbia kisha alijilaza katika miwa asionekane ila kwa msaada wa mbwa waliokuwa wakimkimbiza mtuhumiwa huyo walifanikiwa kumkamata na mara baada ya kumkamata walimkuta akiwa na mfuko wenye mabomu yalizobakia.
Muda mfupi baadae wananchi wenye hasira kali walifika eneo alipokamatiwa mtuhumiwa huyo wakiwa na silaha kali za jadi wakitaka kumuua kijana huyo lakini Polisi waliokuwa wakisaidiana na wananchi hao walifika eneo lile nakumchukua mtuhumiwa huyo.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari(kushoto) na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakimfariji majeruhi.