Tuesday, December 13, 2011

Bi. Shosti afuga nywele miaka 14


Ni Linmei, 55, raia wa China, hajawahi kukata nywele kwa muda wa miaka 14.

Kutokana na hali hiyo, nywele zake zimekuwa kivutio kwenye mitandao, kwani watu kutoka kona mbalimbali duniani wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu.

Akipiga stori na mtandao wa Daily Mail hivi karibuni, Ni Linmei alisema kuwa nywele zake kwa sasa zina urefu wa futi 8.

Alisema kuwa kutunza nywele hizo siyo kazi ndogo na kwamba amekuwa akitumia fedha nyingi kununua shampoo inayomsaidia kuzistawisha.

Alisema, mara nyingi amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kuona nywele zake, jambo ambalo humfanya achukue muda mwingi kuchana na kuzionesha hususan kwenye maonesho ya watalii.

“Ni Linmei amekuwa akipoteza muda mwingi kwenye sofa pasipo kufanya kazi kwa ajili ya kuonesha urefu wa nywele zake,” alisema mtu wa karibu. 

Wanawake wengi huhangaika kujua siri ya mafanikio ya Ni Linmei lakini hata hivyo, hakuna aliyefanikiwa kumfikia mwanamama huyo ambaye akitaka kuonesha nywele zake hupanda juu ya kiti na kuziachia kwa sababu yeye mwenyewe zinamzidi urefu.