Sunday, May 20, 2012

CHELSEA WACHUKUA KOMBE LA UEFA

Chelsea imetwaa ubingwa Ulaya baada ya kuifunga Bayern Munich mikwaju ya penalti 4-3 mchezo wa fainali uliopigwa Allianz Arena. Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za kawaida, Drogba ambaye yuko njiani kutemwa na klabu hiyo kwa kuwa ni 'mzee' alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 83 na kufunga penalti ya mwisho iliyoamua bingwa.
Drogba ni kama nyota wa mchezo ambaye anasema: "Ni jitihada zetu, tulijipanga muda mrefu na sasa matokeo yake yameonekana. Tumecheza kwa tahadhari lakini kwa kujiamini, tuliondoa hofu ya mchezo na tulipambana hadi mwisho.

Ubingwa wa Chelsea ambao ni wa kwanza katika historia ya kombe hilo na klabu, umemaliza hasira za timu hiyo kushindwa katika fainali ya 2008 walipopoteza mechi kwa Manchester United kwa mikwaju ya penalti 6-5 mjini, Moscow Russia.Chelsea iliyokuwa bila nahodha wake, John Terry, anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyozawadiwa kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya Barcelona ilikuwa makini katika mchezo huo licha ya kutangulia kufungwa.

Mpachika mabao mahiri, Thomas Mueller aliifungia Bayern Munich bao la kuongoza katika dakika ya 83. Toni Kroos alipiga mpira kutoka wingi ya kulia na kumchanganya Mario Gomez na Ashley Cole na mpira kumkuta Thomas Mueller aliyeutupia ndani ya kimia. Dakika ya 88, Didier Drogba ambaye anakwenda China kucheza soka ya kulipwa na Nicolas Anelka katika klabu ya Shanghai Shenhua, alifunga kwa kichwa katika dakika ya 88.

Baada ya hapo, zilifuata dakika 120, na waliokuwa wamalize mchezo mapema ni Bayern Munich lakini Arjen Roben alikosa penalti iliyodakwa na kipa Petr Czech. Ilipowadia wakati wa mikwaju ya penalti, Bayern Minich waliotwaa kombe hilo mara nne 1974-76 na 2001, walifunga tatu za kwanza kupitia kwa Philipp Lahm, Mario Gomez na  Manuel Neuer wakati Juan Mata na Bastian Schweinsteiger walikosa.
Walioifungia Chelsea ni David Luiz, Frank Lampard, Ashley Cole na Didier Drogba wakati Ivica Olic alikosa penalti yake. Drogba ndiye aliyesawazisha na kisha kufunga penalti iliyoipa ubingwa timu hiyo.
TIMU ZA ENGLAND ZILIZOWAHI KUWA BINGWA WA ULAYA:
Liverpool (Mara 5)
Manchester United (3)
Nottingham Forest (2)
Aston Villa (1)
Chelsea (1)