WANAFUNZI 9000 WAFUTIWA MATOKEO, HATA WALE
WATAKAOINGIA KIDATO CHA KWANZA KUPIMWA UWEZO TENA

Gedius Rwiza na Raymond Kaminyoge
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba ikieleza kuwa wanafunzi 9000 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na hata wale ambao watapangiwa shule za sekondari wapimwa uwezo wao kabla ya kuanza masomo. Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo pamoja na mambo mengine, alisema kutokana na tatizo hilo, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani, watapaswa kuchujwa upya.