Saturday, October 22, 2011

MZOZO JUU YA MAZISHI YA GADDAFI.

Mazishi ya Kanali Muammar Gaddafi yamesitishwa kutokana na tofauti zilizozuka baina ya maafisa wa Libya kuhusu jinsi ya kufanya maziko hayo. Chini ya utamaduni wa Kiislam, maziko hutakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo. Lakini waziri wa mafuta wa Libya amesema mwili wa Gaddafi huenda ukahifadhiwa "kwa siku kadhaa".Haifahamiki kama kiongozi huyo wa zamani atazikwa Sirte, mji aliouawa siku ya Alhamis, au Misrata, mji aliopelekwa baada ya kufa, au mahala pengine.Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kifo cha Muammar Gaddafi kinamaanisha shughuli za Nato nchini Libya zimefikia kikomo.Awali kulikuwa na taarifa kuwa mamlaka nchini Libya zinafanya mipango ya kufanya mazishi ya siri kwa kiongozi huyo. Hata hivyo, inaonekana huenda kukawa na kuchelewa kufanyika kwa mazishi hayo, ambayo chini ya utamaduni wa Kiislam mazishi hufanyika haraka iwezekanavyo.Waziri wa mafuta Ali Tarhouni aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mwili wa Kanali Gaddafi huenda ukahifhadhiwa "kwa siku kadhaa".

JAMAA ANA WAKE 39, WATOTO 94 NA NYUMBA YENYE VYUMBA 100

Familia yake inaendeshwa kwa utawala unaofanana na kijeshi huku mke mkubwa mwenye umri wa miaka 69 akiwa mpangaji mkuu wa majukumu ya uendeshaji nyumba kwa wenzake , mlo wa siku ni karibu gunia zima la mchele na kuku wapatao 30.
Nyumba ia Ziona ina uwanja wa kuchezea watoto,mabanda ya kufugia wanyama ,shule yake yenyewe na sehemu ya uhunzi. Kuna wakati alioa wake kumi katika mwaka mmoja na chumbani kwake ana sita kwa sita la kufa mtu na kila usiku mke mmoja huwa naye ,hivyo huwachukua kila mtu zaidi ya miezi miwili kwa wake zake kuwa naye faragha ya usiku. vyumba vya wake zake wadogo viko karibu na chumba chambe na walio wazee viko mbali naye.
Ziona na Wake zake
Jumba la ZIONA