Tunaomba radhi kwa picha hii
Mh Lema na Mh Mbowe wakijadili jambo baada ya taharuki
Umati wa wanachama wa Chadema walivyokua wamekusanyika kwenye mkutano huo maeneo ya Soweto jijini Arusha, kabla ya taharuki kutokana na kitu kinachodhaniwa ni mlipuko wa bomu.
Habari za hivi punde zinasema, kumetokea mlipuko wa bomu Arusha maeneo ya Soweto katika mkutano wa CHADEMA. Mkutano huo ulikuwa wa mwisho kabla ya uchaguzi wa madiwani kufanyika hapo kesho.
Mbunge wa Arusha Mjini Mh GodBless Lema alikua pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh Freeman Mbowe katika mkutano huo. Inasadikika watu kadhaa wamefariki dunia na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Arusha Mt Meru na Selian. Huu ni mfululizo wa matukio haya ya mabomu baada ya ule uliotokea Olasiti Mbauda mwezi uliopita hapa hapa jijini Arusha.
Duh jamani Watanzania tuwe na Roho za Ruhuma' mpaka tunafikia hatua kama hizi? tunamalizana wenyewe kwa wenyewe!
We need changes between our selves this is too much
No comments:
Post a Comment