LORD EYEZ
Msanii wa Bongo Fleva kutoka A town city almaarufu kama Lord eyez ambaye siku za hivi karibuni alikabiliwa na kesi ya kuiba vifaa vya gari sasa
Latest Info
ni kwamba msanii huyu pamoja na Wakili wake waliamua kuweka wazi juu ya kesi inayomuanda hivi sasa.Wakili huyu anayekwenda kwa jina la Peter Kibatala
alisema kwamba kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye
ndiyo mhusika wa kuiba vifaa hivyo lakini sasa hivi wanaachia kwanza
Mahakama ndiyo itakayo chukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi
hiyo.Lakini hapo hapo tuliweza kusikia ujumbe kutoka kwa weusi
walizungumza na kusema kwamba tukio kama ili limewaathiri pale
wanapokutana na watu mbalimbali na kusikia story za watu kusema kwamba
wote watakuwa wanahusika katka kesi hiyo wakati ni story ambazo sio za
kweli.Baada ya hapo tuliweza pia kusikia ujumbe kutoka kwa Lord Eyez mwenyewe
aliweza kuzungumza kusema kwamba mahakama ndiyo itaamua kuchukua sheria
kwamba alihusika au ajahusika katika tukio kama hilo la kuiba vifaa vya
gari,ambayo kesi hiyo inatarajia kusomwa Mahakama ya Mwanzo siku ya
tarehe 13,14 na 15 mwezi huu hapa jijini Dar es Salaam lakini
pia alimalizia kwa kusema japokuwa kwa sasa hivi yupo kitaani huku
akisikilizia Mahakama imeamuaje kwa hiyo anachotaka kukifanya ni
anataka kudondosha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya suprise
kwa mashabiki wake katika industries hii ya muziki wa Bongo Fleva.
Nikki wa Pili, Lord Eyez na G nako.