MADRID, Hispania
JOSE Mourinho ameamua kubaki Real Madrid pamoja na kushindwa kufuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo.''Kama klabu na wachezaji wakitaka niendelea, nitaendelea,'' alisema Mourinho baada ya kuishudia Madrid kitolewa kwa penalti 3-1 na Bayern Munich kufutia mchezo huo kumalizika kwa sare ya jumla ya mabao 3-3.
Mourinho pia alitumia nafasi hiyo kuwatetea Cristiano Ronaldo na Kaka wachezaji bora wa zamani wa dunia waliokosa penalti kwa kutolea mfano nyota wa Barcelona, Lionel Messi aliyekosa penalti dhidi ya Chelsea.
''Ni jambo linalonishanganga mimi mnataka watu wasahau kuhusu Messi kukosa penalti muhimu kwa kuwanyooshea vidole wachezaji watatu waliokosa penalti leo,'' alisema.
Madrid sasa macho yake yatakuwa kwenye mbio za kuivua ubingwa Barcelona baada ya misimu mitatu kumaliza nafasi ya pili, na kufanikiwa kutwaa kombe moja tu la Copa del Rey. Madrid inaongoza mbele ya Barcelona kwa pointi saba ikiwa imebaki michezo minne.
No comments:
Post a Comment