Friday, April 27, 2012

REAL MADRID NAYO YAAGA UEFA



MADRID, Hispania
JOSE Mourinho ameamua kubaki Real Madrid pamoja na kushindwa kufuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo.
''Kama klabu na wachezaji wakitaka niendelea, nitaendelea,'' alisema Mourinho baada ya kuishudia Madrid kitolewa kwa penalti 3-1 na Bayern Munich kufutia mchezo huo kumalizika kwa sare ya jumla ya mabao 3-3.

Mourinho pia alitumia nafasi hiyo kuwatetea Cristiano Ronaldo na Kaka wachezaji bora wa zamani wa dunia waliokosa penalti kwa kutolea mfano nyota wa Barcelona, Lionel Messi aliyekosa penalti dhidi ya Chelsea.
''Ni jambo linalonishanganga mimi mnataka watu wasahau kuhusu Messi kukosa penalti muhimu kwa kuwanyooshea vidole wachezaji watatu waliokosa penalti leo,'' alisema.
Madrid sasa macho yake yatakuwa kwenye mbio za kuivua ubingwa Barcelona baada ya misimu mitatu kumaliza nafasi ya pili, na kufanikiwa kutwaa kombe moja tu la Copa del Rey. Madrid inaongoza mbele ya Barcelona kwa pointi saba ikiwa imebaki michezo minne.

Wednesday, April 25, 2012

CHELSEA YAITOA BARCELONA UEFA


KATIKA kile kinachoonekana kumalizika kwa utawala wa Barcelona, mabingwa hao wa tetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wametolewa katika michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Chelsea kwenye Uwanja wa Camp Nou, jana.
Kutokana na matokeo hayo Barcelona imevuliwa ubingwa rasmi na hivyo Chelsea imefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-2, kutokana na ushindi wa Chelsea wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Chelsea ilicheza muda mwingi ikiwa pungufu baada ya nahodha wake, John Terry kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 37 kutokana kumgonga Alexies Sanchez.
Chelsea ambayo ilitumia muda mwingi ikilinda lango lake ilipata mabao yake kupitia kwa Ramires na Fernando Torres, wakati  Barcelona ilipata mabao yake kupitia Sergio Busquets na Andres Iniesta.
Kipindi cha pili Barca ilipata penalti katika dakika ya 49, lakini Lionel Messi, aligongesha mwamba na mpira kuokolewa.
Torres aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Didier Drogba, ndiye aliyehitimisha safari ya Barca kutokana na bao lake katika dakika ya 90.
Kutokana na matokeo hayo, Chelsea inasubiri mshindi wa mchezo ya leo kati ya Real Madrid dhidi ya Bayern Munich.

Monday, April 23, 2012

VAN PERSIE WINS PFA AWARD


Arsenal striker Robin van Persie has been named the Professional Footballers' Association Player of the Year Award  (PFA).
The 28-year-old Holland international has scored 27 Barclays Premier League goals this season for Arsène Wenger's side - his most fruitful campaign for the Club - and was humbled to be recognised by his peers.
"If other people are saying it, it is special, but it is even more special if your opponents are saying it," he told Press Association Sport.

Thursday, April 19, 2012

WATENGWA TO FRANCE TOUR

Group ya wakali wa Hip Hop kutoka Arusha
"Watengwa" wanatarajiwa kwenda Ufaransa
kwenye Tamasha linalofahamika kama
 “Festiv’ Al Arrach” litakalo husisha wasanii
 kutoka sehemu mbali mbali duniani ikiwemo
 familia ya Watengwa from Arusha wao kama
 wahusika wakuu, Ni Tamasha ambalo linalenga
kupromote utamaduni wa Afrika mashariki.
Taasisi iliyoandaa tamasha hilo inaitwa UUKSA,
Tamasha hilo litafanyika mwezi mzima, Watengwa
 watakua na studio sessions, Radio Interviews pamoja
na kutengeneza Documentary na kurekodi album ya
 Full Ile Laana Vol.2.

Thursday, April 12, 2012

ALL STAR

This is my favourite shoes in town
"ALL   STAR   CONVERSE"

SAFARI YA MWISHO YA STEVEN KANUMBA

Maazishi ya msanii wa filamu, aliyebeba mapenzi makubwa ya Watanzania, Waafrika na dunia kwa jumla, Steven Charles Kanumba aliyefikwa na umauti ghafla usiku wa Aprili 6, 2012, na kuzikwa tarehe 10/04/2012 katika Makaburi ya Kinondoni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.Kifo chake kilisababishwa kutokana na kusukumwa na mpenzi wake msanii mwenzake Elizabeth Michael maarufu kama LuLu, na kusababisha kugonga sehemu ya kichwa na kufanya mtingishiko wa ubongo unaojulikana kitaalam kama BRAIN CONCUSSION.
we will always remember you bro!
REST IN FREEDOM