Saturday, March 23, 2013

NIKKI WA PILI AELEZEA MAFANIKIO YA NGOMA ZAKE "BUM KUBAM" NA "NJE YA BOX"

The best Rapper kutoka kampuni ya weusi A town Tanzania
 Nikki wa Pili ameelezea mistari aliyoandika kwenye
single yake mpya nje ya boksi pamoja na mafanikio
aliyoyapata baada ya kuuza DVD ya kubumkubam.
Kupitia One2One Interview iliyokuwa hosted na Dulla Ambua
kwenye kipindi cha Planet Bongo Eat Africa Tv jana usiku
Nikki wa Pili alisema kwamba wakati alipo compose wimbo ya
 nje ya Boksi lengo lake ilikuwa ni kuandika mapenzi katika
 uhalisia sio nadharia.
Mkali huyo alisema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja mafanikio
 aliyopata kwenye mauzo ya DVD ya Kubumkubam
kupitia mtandao akishirikiana na kampuni ya
 fichuka ni nakala 745.

Akiwa kama msanii na msemaji wa WEUSI' Nikki alisema wiki ijayo itatoka video ya Joh Makini inayoitwa Kiutu Uzima na week end hii G Nako ata shoot video ya Mama Yeyo' huku Lord Eyez akisubiri  kutoa video ya Baba la Baba ft Ben Pol - No more Drama ambayo ame shoot na wa Denmark.

No comments:

Post a Comment