JESHI la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya
marehemu Hussein Ramadhan, ‘Sharo Milionea’ vilivyoibwa na watu
wasiojulikana, muda mfupi baada ya msanii huyo wa filamu na muziki
nchini kupata ajali katika Kijiji cha Songa Kibaoni, wilayani Muheza na
kufariki dunia papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,
Costantine Massawe alisema Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata begi
la nguo, simu ya mkononi aina ya blackberry, betri ya gari, redio, tairi
la gari na saa ya mkononi ya marehemu.
Alitaja vitu vingine vilivyopatikana kuwa ni nguo ambazo marehemu
alivuliwa baada ya kupata ajali, ambazo ni fulana na suruali ya jeans.
No comments:
Post a Comment