Tuesday, December 25, 2012
Wednesday, December 12, 2012
Tuesday, December 4, 2012
PAPA BENEDICT AJIUNGA NA MTANDAO WA TWITTER
Papa Benedict amefungua akaunti katika mtandao wa kijamii,Twitter, katika jitihada ya kusambaza ujumbe wa kanisa katoliki.
Taarifa kuhusu akaunti hiyo itatolewa baadaye
hii leo katika mkutano na waandishi habari, lakini duru kutoka Vatican
zinasema huenda asiandike mwenyewe ujumbe kwenye akaunti hiyo.Wanasema Papa Benedict anapendelea kuandika kwa mkono kuliko kutumia tarakilishi.
Kanisa hilo la katoliki tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni limezindua mtandao mkuu unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.
Wakatoliki kote duniani, wataweza kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo itakapozinduliwa rasmi.
Papa Benedict anataka kuitumia akaunti hiyo kuwasiliana na wakatoliki kote duniani.
Saturday, December 1, 2012
VITU VYA SHARO MILIONEA VILIVYOIBIWA VYAKAMATWA
JESHI la Polisi mkoani Tanga limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya
marehemu Hussein Ramadhan, ‘Sharo Milionea’ vilivyoibwa na watu
wasiojulikana, muda mfupi baada ya msanii huyo wa filamu na muziki
nchini kupata ajali katika Kijiji cha Songa Kibaoni, wilayani Muheza na
kufariki dunia papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,
Costantine Massawe alisema Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata begi
la nguo, simu ya mkononi aina ya blackberry, betri ya gari, redio, tairi
la gari na saa ya mkononi ya marehemu.
Alitaja vitu vingine vilivyopatikana kuwa ni nguo ambazo marehemu
alivuliwa baada ya kupata ajali, ambazo ni fulana na suruali ya jeans.
Subscribe to:
Posts (Atom)