Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma Kaseja Juma kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo.
Kikosi cha Simba Football Club
Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza.nGoli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari.
No comments:
Post a Comment