Baada ya miaka 44 hatimaye Man City wamechukua ubingwa wa England 2012 maarufu kama English Premier League, baada ya kuifunga Queens Park Rangers magoli 3-2. Mshambuliaji Sergio Aguero alifunga bao la tatu na ushindi katika dakika za majeruhi na kurudisha shangwe za mashabiki wa City uwanjani hapo.
Zabaleta alifunga bao la kwanza kabla ya Edin Dzeko na Aguero waliokuwa mashujaa wa City kwenye uwanja wake wa Etihad kufunga mabao. "Kushinda kwa aina hii ni kitu kizuri. Sijawahi kuona mechi ya mwisho ngumu kama hii. Baada ya miaka 44 tumefanikiwa kutoa zawadi kwa mashabiki wetu wote," alisema kocha wa City, Roberto Mancini.

No comments:
Post a Comment