Saturday, October 22, 2011

JAMAA ANA WAKE 39, WATOTO 94 NA NYUMBA YENYE VYUMBA 100

Familia yake inaendeshwa kwa utawala unaofanana na kijeshi huku mke mkubwa mwenye umri wa miaka 69 akiwa mpangaji mkuu wa majukumu ya uendeshaji nyumba kwa wenzake , mlo wa siku ni karibu gunia zima la mchele na kuku wapatao 30.
Nyumba ia Ziona ina uwanja wa kuchezea watoto,mabanda ya kufugia wanyama ,shule yake yenyewe na sehemu ya uhunzi. Kuna wakati alioa wake kumi katika mwaka mmoja na chumbani kwake ana sita kwa sita la kufa mtu na kila usiku mke mmoja huwa naye ,hivyo huwachukua kila mtu zaidi ya miezi miwili kwa wake zake kuwa naye faragha ya usiku. vyumba vya wake zake wadogo viko karibu na chumba chambe na walio wazee viko mbali naye.
Ziona na Wake zake
Jumba la ZIONA


1 comment: