Familia ya Mr Ebbo, ndugu jamaa na marafiki
Wazazi wa Mr Ebbo wakiwa na Mbunge wa zamani na Waziri wa Mazingira, Dr Batilda Buriani.
Watoto Watatu wa Mr Ebbo wakifarijiwa na ndugu
Maelfu ya wakazi wa mjini Arusha na nje ya mji wa Arusha wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Mr Ebbo.
Wananchi hao ambao walikuwa na shauku ya kuuaga mwili wa marehemu huyo walijitokeza kwa wingi huku wakionekana kuwa na nyuso za majonzi, kila mmoja akihuzunika na wengi wakidai kuwa mwimbaji huyo wa bongo flava ameacha pigo kubwa kwa jamii ya kimasai na Taifa kwa ujumla kwani muziki wake sambamba na kuburudisha ulikuwa unaelimisha kwa kiwango kikubwa.
Akiongea katika mazishi hayo askofu mkuu wa jimbo la kaskazini Thomas Laizer alisema kuwa wao kama kanisa limeupokea msiba huo kwa masikitikio makubwa kwani msanii huyo alikuwa anaelimisha jamii kupitia nyimbo zake pia aliweza kuutangaza mkoa wa Arusha pamoja na kabila la kimasai kupitia nyimbo zake.
.........REST IN PEACE MR EBBO.......
No comments:
Post a Comment