Wednesday, December 28, 2011

MAFURIKO YAHAMIA MJI WA MOROGORO

Hali ilikuwa mbaya kwa waliolazimika kupata mahitaji yao sokoni hapo.
BAADA ya jiji la Dar es Salaam kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo vya makumi ya watu na kuharibu nyumba nyingi za wakazi wa jiji hilo, mchana wa leo hali hiyo imehamia mkoani Morogoro ambapo baadhi ya nyumba za watu, likiwemo soko kuu la Manispaa ya Morogoro yamekumbwa na mafuriko makubwa kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa muda wa dakika 45 mfululizo.

Thursday, December 15, 2011

MITIHANI YA DARASA LA SABA YACHAKACHULIWA

WANAFUNZI 9000 WAFUTIWA MATOKEO, HATA WALE
WATAKAOINGIA KIDATO CHA KWANZA KUPIMWA UWEZO TENA 

Gedius Rwiza na Raymond Kaminyoge
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba ikieleza kuwa wanafunzi 9000 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na hata wale ambao watapangiwa shule za sekondari wapimwa uwezo wao kabla ya kuanza masomo.  Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo pamoja na mambo mengine, alisema kutokana na tatizo hilo, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani, watapaswa kuchujwa upya.

WANAFUNZI 43 WATIMULIWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimewafukuza wanafunzi 43 na kuendelea kufuatilia nyendo za wengine tisa, baada ya kubainika kuwa walihusika katika matukio mbalimbali ya vurugu na uhalifu chuoni hapo. Kati ya wanafunzi hao, wanane walikuwa wamesimashiwa masomo kwa muda wa miezi tisa na 35 walisimamishwa ili kusubiri kumalizika kwa kesi zao zilizopo mahakamani.

DAH SNOOP DOG APIGA MSUBA JUKWAANI


MWISHO & MERYL WAFUNGA PINGU ZA MAISHA NCHINI NAMIBIA


Tuesday, December 13, 2011

Bi. Shosti afuga nywele miaka 14


Ni Linmei, 55, raia wa China, hajawahi kukata nywele kwa muda wa miaka 14.

Kutokana na hali hiyo, nywele zake zimekuwa kivutio kwenye mitandao, kwani watu kutoka kona mbalimbali duniani wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu.

Akipiga stori na mtandao wa Daily Mail hivi karibuni, Ni Linmei alisema kuwa nywele zake kwa sasa zina urefu wa futi 8.

Alisema kuwa kutunza nywele hizo siyo kazi ndogo na kwamba amekuwa akitumia fedha nyingi kununua shampoo inayomsaidia kuzistawisha.

Alisema, mara nyingi amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kuona nywele zake, jambo ambalo humfanya achukue muda mwingi kuchana na kuzionesha hususan kwenye maonesho ya watalii.

“Ni Linmei amekuwa akipoteza muda mwingi kwenye sofa pasipo kufanya kazi kwa ajili ya kuonesha urefu wa nywele zake,” alisema mtu wa karibu. 

Wanawake wengi huhangaika kujua siri ya mafanikio ya Ni Linmei lakini hata hivyo, hakuna aliyefanikiwa kumfikia mwanamama huyo ambaye akitaka kuonesha nywele zake hupanda juu ya kiti na kuziachia kwa sababu yeye mwenyewe zinamzidi urefu.

Wednesday, December 7, 2011

I LIKE THIS ONE JHAMANI.....!

My Life, My Choices... My Mistakes, My Lesson... and not your business!

MR EBBO AZIKWA NYUMBANI KWAO ARUSHA

Familia ya Mr Ebbo, ndugu jamaa na marafiki


Wazazi wa Mr Ebbo wakiwa na Mbunge wa zamani na Waziri wa Mazingira, Dr Batilda Buriani. 

Watoto Watatu wa Mr Ebbo wakifarijiwa na ndugu

Maelfu ya wakazi wa mjini Arusha na nje ya mji wa Arusha wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Mr Ebbo.

Maelfu ya wananchi wamejitokeza kwa wingi mjini Arusha katika safari ya mwisho ya msanii wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava) Abeili Motika almaarufu kwa jina la Mr. Eboo ambaye amezikwa kwenye makaburi ya ukoo nyumbani kwa mzee Lotiko. 


Wananchi hao ambao walikuwa na shauku ya kuuaga mwili wa marehemu huyo walijitokeza kwa wingi huku wakionekana kuwa na nyuso za majonzi, kila mmoja akihuzunika na wengi wakidai kuwa mwimbaji huyo wa bongo flava ameacha pigo kubwa kwa jamii ya kimasai na Taifa kwa ujumla kwani muziki wake sambamba na kuburudisha ulikuwa unaelimisha kwa kiwango kikubwa. 


Akiongea katika mazishi hayo askofu mkuu wa jimbo la kaskazini Thomas Laizer alisema kuwa wao kama kanisa limeupokea msiba huo kwa masikitikio makubwa kwani msanii huyo alikuwa anaelimisha jamii kupitia nyimbo zake pia aliweza kuutangaza mkoa wa Arusha pamoja na kabila la kimasai kupitia nyimbo zake.
.........REST IN PEACE MR EBBO.......