Friday, November 18, 2011

UPUUZI WA MASOUD KIPANYA

UPUUZI WA MASOUD KIPANYA ni documentary ya dakika 47 ambayo nimeirekodi mwaka juzi katika mazingira ya kijiji kilichotumika kurekodia MAISHA PLUS.
Mfumo nilioutumia ni kuongelea mambo mengi mchanganyiko na ili kuondoa uchovu wa kunitazama nikiongea, nimechanganya footages za videos, illustrations na animation (katuni)  kuchagiza yale ninayokuwa nayazungumzia.
Ujumbe wa dvd hii ni nadharia ya vipande 26 vya keki. nikatengeneza MFANO wa uwepo wa idadi hiyo ya vipande vya keki ambavyo mara baada ya kuwekwa mbele ya watu (watanzania), kundi hilo la watu likataka kutoana roho ili kila mmmoja apate kipande cha keki hiyo, bahati nzuri wakatokea werevu (viongozi) ambao waling'amua kuwa kumbe idadi ya vipande vya keki (26) ni sawa kabisa na idadi ya watu waliokuwepo ambao walikuwa wanakaribia kutoana roho.
Werevu hawa wakawaambia watu hawa kuwa hatuna haja ya kung'oana meno wakati idadi yetu ni sawa kabisa na vipande vilivyopo, ukatengenezwa uataratibu wa kupanga foleni ili kila mmoja apite mbele achukue KIPANDE chake. baada ya kukubaliana hilo, bado werevu wakaona ni vema foleni hii iangalie walio dhaifu ili wawe mbele wawahi kupata keki kuchelea kuanguka kwa njaa.
Wakati vipande hivi vya keki vilipoanza kugawiwa, hawa viongozi, (watatu) wakaamua nao kwa kuwa ni sehem ya watu 26 kuchukua VIPANDE VYAO MAPEMA, bahati mbaya baadhi yao kutokana na kuwa karibu na meza ya keki na kutokana na ULAFI, wakaamua kuchukua zaidi ya kipande kimoja cha keki hali iliyopelekea watu wa mwishoni katika foleni ile kukosa vipande vyao.
Dvd hii pia imeingia ndani kwa mafumbo kiasi kuangalia sababu inayopelekea watu kutaka kujipendelea zaidi kiasi cha kupelekea kudhulumu  wengine, ikajaribu pia kuangalia dawa inayoweza kutumiwa kuepuka hali hii ya uchu na tamaa inayosababishwa na hofu ya kujiuliza nitapata lini na woga wa kuhofia kupoteza kidogo alicho nacho mkononi.


Kwanini umeitwa upuuzi? kwa sababu ya tabia na hulka za binaadam kupenda kupuuza kila kitu, ni hili nalo limetengenezwa ili ulitazame kisha ulipuuze.
Concept: Ni documentary yenye sauti na picha za video pamoja na katuni mnato na katuni mtembeo (still cartoons and animation) 
Wahusika wakuu: Masoud Kipanya
Itaingia lini sokoni: imeingia sokoni jana jumanne tarehe 15-11-2011 na inasambazwa na UMOJA AUDIO VISUAL.
Bei: Shilingi 3,000 tu.
Running time: Dakika 47
Sponsors: Hakuna mdhamini.
Future plans: Ni matayarisho ya upuuzi mwingine "WENYE NGUVU NA WAPAGAZI"
Nashukuru kwa ushirikiano wenu na mungu awabariki sana.

MASOUD KIPANYA.


No comments:

Post a Comment