Friday, November 25, 2011

WANA WA A-TOWN, R CHUGGA

United   Streets of  Olmatejoo

Brand New Hip Hop Management are artist and their coming soon from the one streets of Matejoo R chugga this time to bring our hood Front Jah Bless the Streets hope. Also dont miss the T-shirts are coming soon.

HAYA WAPIGA CHABO DARASANI MMPOOOO?

Walimu wa shule moja barani Africa waliamua kuja na mbinu ya kuwadhibiti wanafunzi wasiopenda kujishughulisha na kutegemea kupiga chabo a.k.a kuigilizia darasani wakati wa mitihani.

EMBU TAZAMA MAJALALA YA WENZETU YALIYVO

Haya ni mazingira ya Jalalani pasafi hivi, wenzetu kweli wanajipenda na wanapenda mazingira yao pia' sio kama sisi wabongo tunatupatupa tu na kutokujali mazingira yetu. Bongo hapa watu wameshajichukulia Mafriji hapa.

Thursday, November 24, 2011

MWANAMME ALIYEJIGEUZA DEMU AZUA HOFU DUNIANI


ONEAL Morris, dume  aliyebadili jinsi yake amezua hofu duniani kufuatia picha zake za kwenye mtandao zikimwonesha ni mwanamke, ‘pyua’.
Baadhi ya watu waliotoa maoni kwenye mtandao ulioanika picha za Oneal wamesema wanaamini dunia imefika ukingoni na sasa ni wakati wa bindamu kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

WANAFUNZI WAKODI MABASI KWENDA SHOO YA SUGU.....

SHOO ya uzinduzi wa mix-tape ya Anti Virus inazidi kubamba, upo uwezekano ikajaza nyomi ambalo halijawahi kutokea kutokana na ahadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kwamba watakodi mabasi kwenda kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar.

Anti Virus itasababishwa na Vinega Novemba 26, 2011, kuanzia saa 12 jioni mpaka 6:00 usiku na katika kuhakikisha wanashuhudia makamuzi ya maana, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, wameahidi kukodi m
abasi matatu ya kuwasafirisha kwenda kwenye shoo hiyo.


INABIDI TUKIMBIE WAKATI WENGINE WAKITEMBEA....

Lakini pia ni lazima tukumbuke kwamba wakimbiao huchoka mapema kuliko watembeao, na kama ni mbio za masafa marefu na wakimbiaji hawa wakawa hawajajiandaa na kuchunguzwa afya zao vizuri ipo hatari ya kupata mshtuko wa moyo na kufikwa na umauti wa ghafla. Ati kama ni lazima tupige mbio, sisi tumejiandaaje? Tunajua tuendako? Basi tusije tukakurupuka na kuanza kupiga mbio kama wendawazimu!

Tuesday, November 22, 2011

MUIGIZAJI WA NIGERIA, AKI KUFUNGA NDOA DECEMBER MWAKA HUU

......MR & MRS TO BE.......

Msanii mchekeshaji kutoka Nigeria anatarajiwa kufunga ndoa na Sweetheart wake Nneoma Nwaijah,ambaye amehitimu Enugu State University of Technology,tarehe 10 mwezi december mwaka huu, ndoa ambayo itatanguliwa na ndoa ya kimila mwezi November.

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI AKA MR. SUGU AZUNGUMZA NA WANAHABARI

Waziri kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kulia) Joseph Mbilinyi a.k.a Mr, SUGU akionyesha kitabu ambacho ameelezea maisha yake kitakachopatikana wakati wa Shoo ijulikanayo Anti Virus katika Tamasha la Burudani kwa washabiki2011 litaakalofanyika Nov. 26,2011 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa michezo, (kushoto) ni Msanii Fred Malaki a.k.a. MKOLONI. ( _Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO,)

Waziri kivuli wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Joseph Mbilinyi (a.k.a. MR. SUGU -alievalia kadeti) leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 21-nov-2011 kuhusu shoo ijulikanyo Anti Virus wakati wa Tamasha la Burudani kwa washabiki 2011-i litalaofanyika jijini DSM hapo Nov. 26 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi,(kushoto) ni Msanii Fred Malaki (a,k,a- MKOLONI) n a Mwanadada Zainab Lipangile a.k.a ZAY –B, Katika tamasha hilo Wasanii mbalimbali watatumbuiza, -Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO,

Msanii Suma g akiimba mbele ya wana habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam jana.



Friday, November 18, 2011

UPUUZI WA MASOUD KIPANYA

UPUUZI WA MASOUD KIPANYA ni documentary ya dakika 47 ambayo nimeirekodi mwaka juzi katika mazingira ya kijiji kilichotumika kurekodia MAISHA PLUS.
Mfumo nilioutumia ni kuongelea mambo mengi mchanganyiko na ili kuondoa uchovu wa kunitazama nikiongea, nimechanganya footages za videos, illustrations na animation (katuni)  kuchagiza yale ninayokuwa nayazungumzia.

Friday, November 11, 2011

WAAOH THE AMAZING DATE OF TODAY PEOPLE'S 11/11/11....!

Thanks GOD am doing greets until this day.

MBEYA VURUGU TUPU MAENEO YA SOWETO....!

Mbeya hapafai ni vurugu tupu Wamachinga na Polisi

Baadhi ya WAMACHINGA wakiwa wamelipindua gari aina ya
Toyota na kusimama juu yake wakisumbuana na Polisi


Wazee wakazi FFU mzigoni wakisumbuana na Wamachinga.

njia imezibwa na wakawasha moto katikati ya barabara

Tuesday, November 8, 2011

VIZURI LAKINI NI HATARI.....!

Mmmh

Jamaa sijui kalala usingizi kabisa

Brother hana cha Helmet wala nn.
Mashindano yalikuwa uwanja wa saba saba mjini Morogoro

ANASWA NA UMEME AKIIBA MAFUTA YA TRANSFOMA

Mtu mmoja ambaye hajatambulika jina lake amenaswa na umeme wa transfoma usiku wa kuamkia leo katika eneo la Hospitali ya Bugando jijini Mwanza na kufariki dunia papo hapo.
  Taarifa za uchunguzi zinamtaja mtu huyo ambaye inasemekana kuwa alikuwa katika mchakato wa kuiba mafuta ya transfoma hilo, wakati akifanya wizi huo alinasa mara baada ya kuegemea bila kujua moja ya nyaya zilizokuwa na umeme.

Mafundi wa umeme kutoka Tanesco wakipanda kuunasua mwili wa jamaa huyo.

Asubuhi ya leo mashuhuda kutoka sehemu mbalimbali walimiminika kwenye tukio hilo la kutisha na kuona hatua kwa hatua za ushushaji wa mwili wa mwizi huyo wa mafuta ya transfoma.

TANESCO kupitia kitengo chake cha usalama, kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu hali hiyo, ili kupambana na wizi huo na licha ya kuwakamata baadhi ya wahalifu ambao baadhi yao walifikishwa mahakamani na kesi zao bado zinaendelea kusikilizwa kwenye mahakama mbalimbali hapa nchini bado wizi unafumuka kwa kasi tena ya ajabu chanzo kikuu kikitajwa kuwa ongezeko la mahitaji.

Kila kukicha TANESCO imekuwa ikingia gharama katika kununulia vifaa vilivyoibwa badala ya kuendeleza maendeleo ya miradi ya umeme nchini.
Kutokana wizi huo baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza hususani eneo la Hospitali ya Bugando na maeneo yake ya jirani yamekosa umeme usiku mzima hadi leo na baadhi ya shughuli kusimama kwa kukosa nishati ya umeme.

Monday, November 7, 2011

REDD'S UNI FASHION BASH AT MOSHI......

Washindi wa shindano la Redd's Uni Fashion Bash mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa washindi. Na kuhudhuriwa na mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoani humo.

Baadhi ya washiriki wa shindano hilo wamejipanga jukwaani......!

Moja kati ya burudani zilizotolewa ni kundi la sarakasi na kuwa kivutio kikubwa pamoja na mkali wa Hip Hop Joh Makini.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya mkoani Kilimanjaro 
wakiendelea kutazama shindano la Redd's Uni Fashion Bash.
Tamasha hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Glaciers - Shanty 
Town mjini Moshi hivi majuzi.

Friday, November 4, 2011

WARAKA WA MH. GODBLESS LEMA KWA WATANZANIA JUU YA KWENDA KWAKE JELA...


WAARUSHA NA WATANZANIA WAPENDA
MABADILIKO KOKOTE KULE WALIPO ULIMWENGUNI
JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.
Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu.
Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.