Monday, October 24, 2011

MAN U YAPATA KIPIGO 6-1 DHIDI YA MAN CITY

MANCHESTER UNITED JUMAMOSI ILIGEUKA NA KUWA MANSITA
Baada ya kupokea kichapo toka kwa mahasimu wao Manchester city, kwenye uwanja wao wa nyumbani Old Trafford  OT.

Mchezo wa Manchester United umeacha majonzi makubwa si tu katika jiji la Manchester bali ni kwa wapenzi wa timu hiyo walioko dunia nzima waliposhuhudia bila kuamini timu yao ikichapwa mabao 6-1 huku Mario Balotelli akipachika magoli mawili.
Sergiao aliongeza bao la tatu kwa Man City na kuimarisha ushindi wao wa kishindo kwenye uwanja huo tangu waliposhinda 6 -1 January 1926.
David Silva alifunga la nne huku mawili ya mwisho yakipachikwa na Edin Dzeko, na Man U walipata la kufutia machozi lililowekwa kambani na Fletcher. Hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa Jonny Evans wa United kupewa kadi nyekundu.

1 comment: