Monday, June 11, 2012

WAZIRI SAITOTI NA NAIBU WAKE WAFARIKI DUNIA

Profesa George Saitoti enzi za uhai wake

Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi. Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika. Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijabainika.
Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong. Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.

Friday, June 8, 2012

DJ FETTY HUYOOO BBA THIS WEEK END


DJ Fetty will be the DJ for the Big Brother Saturday Night Party as well as for the Eviction Show.
Famous as Dj Fetty, My name is Fatma Hassan born and raised in Tanzania, started deejaying in 2006 as an employee at Clouds Fm radio station in Dar-es-Salaam on a very popular afternoon show (Dr Beat) by then, playing mostly hip hop, r&b, Bongo Fleva and a little bit of pop, while on the show I joined Clouds dj group (Nyuki dj’s) in a phenomena show at the time (Saturday night live) every Saturday, performing in different regions every weekends including Mwanza, Tanga and Dodoma it is this time I started gaining popularity becoming the only female best dj in Tanzania to date. Performed at the biggest yearly musical event (Fiesta) three years in a raw 2009 – 2011 as well as on MTV VJ search 2007 in Arusha. Still working with Clouds Fm Radio as dj, presenter (clouds top 20) and producer.

Thursday, June 7, 2012

CHILAX WITH MATES

TAWI LA CHADEMA WASHINGTON DC

Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake  Mhe. Libe Mwang'ombe akimkabidhi rasmi mwanachama  ambaye ni mwana mitindo Linda  Bezuidenhout (LB) katika ofisi ya  tawi la Chadema Washington DC.

Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe.  Kalley pamoja na katibu wake  Mhe. Libe Mwang'ombe wakipata picha ya pamoja na Linda  Bezuidenhout Atlanta, Georgia na wanachama wa tawi la chadema Washington DC

Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata Champagne